BIBLIA YASEMA
Would you like to react to this message? Create an account in a few clicks or log in to continue.

Go down
avatar
Admin
Admin
Posts : 8
Join date : 2018-02-03
https://biblia-yasema.board-directory.net

Sifa za wakili Empty Sifa za wakili

Sat Feb 03, 2018 5:29 pm
Sifa za Wakili

SABATO MCHANA

Soma Kwa Ajili ya Somo la Juma Hili:Ebr. 11:8–12 Warumi 4:13, 18–21; Mathayo 6:24; Ebr. 9:14; 1 Yohana 5:2, 3; Luka 16:10–12.

Fungu la Kukariri: “Mtu na atuhesabu hivi, kuwa tu watumishi wa Kristo, na mawakili wa siri za Mungu. Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu”(1 Wakorintho 4:1, 2).


Mawakili wanafahamika kwa chapa yao, au alama yao bainishi, sawa kama vile wauzaji wa rejareja wa bidhaa wanavyofahamika kwa nembo au jina la bidhaa. Kwa kweli, watu wengi wamekuwa maarufu kwa kujigeuza wenyewe kuwa chapa inayouzika.

Chapa, au alama ya wakili wa Kikristo, ni kuakisi upendo wa Kristo kupitia katika uhusiano alio nao pamoja naye. Tunapoishi na kutenda sifa bainishi za Kristo, maisha yetu yatadhihirisha chapa yetu. Chapa yetu ndio chapa yake; au utambulisho wetu umeunganishwa pamoja na wake (1 Wakorintho 6:17).

Juma hili tunaangalia katika kutambulisha sifa bainishi za tabia za mawakili wa Mungu ambazo zinafanya jina lao la bidhaa. Sifa hizi bainishi zinatutia moyo kuutarajia ujio wa Yesu na kutenda kazi tuliyokabidhiwa kama mawakili waaminifu wa ukweli wake. Kila sifa huelezea uhusiano wa kina tunaoweza kuwa nao pamoja na Yeye aliyekuja kutafuta na kuokoa waliopotea. Kadiri ambavyo sifa hizi zinachunguzwa, ndivyo zitakavyojengeka kwa kina zaidi katika maisha yetu. Tabia ya Mungu ya upendo, katika uwezo wake wote, utakuwa ni chapa yetu na kuwa na mvuto katika kila kipengele cha maisha yetu, leo na milele.

*Jifunze somo la juma hili ukijiandaa na Sabato ya Februari 10.



avatar
Admin
Admin
Posts : 8
Join date : 2018-02-03
https://biblia-yasema.board-directory.net

Sifa za wakili Empty Re: Sifa za wakili

Sat Feb 03, 2018 5:30 pm
Karibu kwa hoja na mchango juu ya somo hili la lessoni katika siku hii .
Back to top
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum