BIBLIA YASEMA
Would you like to react to this message? Create an account in a few clicks or log in to continue.

Go down
avatar
Admin
Admin
Posts : 8
Join date : 2018-02-03
https://biblia-yasema.board-directory.net

Lesson Jumapili tar4/2.2018- uaminifu Empty Lesson Jumapili tar4/2.2018- uaminifu

Sun Feb 04, 2018 11:04 am
Uaminifu


“Hapo tena inayohitajiwa katika mawakili, ndiyo mtu aonekane kuwa mwaminifu.” (1 Wakorintho 4:2). Kupigana na kushinda “vita vile vizuri vya imani” (1 Timotheo 6:12) ni muhimu kwa wakili mwaminifu. “Mwaminifu” ndivyo Mungu alivyo na ndivyo tunavyopaswa kuwa kupitia kwa utendaji wake ndani yetu. Kuwa mwaminifu humaanisha kudumu kuwa wakweli kwa kile tunachokifahamu kuwa ni sahihi, hasa katika joto la vita vya kiroho.

Mapambano ya kiroho baina ya uadilifu na ubaya, wema na uovu, ni lazima yatakuja. Ni sehemu ya vita vya imani. Uamuzi unaowatambulisha mawakili katika kila hali ni uamuzi wa kuwa mwaminifu. Iwapo unapenda mali, hakikisha unabaki kuwa mwaminifu kwa Mungu na kile anachokisema kuhusu unyenyekevu. Iwapo unapambana na mawazo ya tamaa, dumu kuwa mwaminifu kwa ahadi za utakatifu. Iwapo unataka mamlaka, dumu kuwa mwaminifu kuhusu kile ambacho Mungu anasema juu ya kuwa mtumishi wa wote. Uchaguzi wa kuwa mwaminifu au kutokuwa mwaminifu mara nyingi hufanywa katika kufumba na kufumbua, hata kama matokeo yake yanaweza kuwa ni ya milele.

Soma Waebrania 11:8-12, 17-19, na Warumi 4:13, 18-21. Maandiko haya yanatufundisha nini kuhusu kuwa mwaminifu?

Katika Kiebrania “mwaminifu” humaanisha kutumaini. Mzizi huo huo wa Kiebrania hutupatia neno “amina,” na kwa hakika humaanisha kuwa “yabisi/gumu” au “thabiti/madhubuti.” Uaminifu humaanisha tumepimwa na kujaribiwa, na tumebakia kwa uthabiti kuwa na msimamo katika mpango wa Mungu.

Akijiandaa kuzungumza mbele ya mfalme, Mwanamatengenezo Martin Luther “alisoma neno la Mungu, alipitia maandiko yake, na kutaka kuandika jibu lake kwa jinsi inayofaa. … Alisogea karibu na Maandiko matakatifu … na kwa mhemuko aliweka mkono wake wa kushoto juu ya kitabu kitakatifu, na huku akinyosha wa kulia juu mbinguni, aliapa kwamba angebakia kuwa mwaminifu kwa injili, na kwa kukiri imani yake kwa uhuru, hata kama ingelazimu kutia mhuri ushuhuda wake kwa damu yake.” —J. H. Merle d’Aubigné, History of the Reformation (New York: The American Tract Society, 1846), vol. 2, book 7, uk. 260.


Soma Ufunuo 2:10. Maneno yahusuyo kuwa “mwaminifu hata kufa” yanamaanisha nini kwetu katika kutembea kwetu kila siku pamoja na Bwana?



Karibu kwa mjadala
avatar
Admin
Admin
Posts : 8
Join date : 2018-02-03
https://biblia-yasema.board-directory.net

Lesson Jumapili tar4/2.2018- uaminifu Empty Re: Lesson Jumapili tar4/2.2018- uaminifu

Sun Feb 04, 2018 3:05 pm
Uaminifu ni mtaji sana kwa wanadamu, japo ni kazi ila tunaweza kushinda, na kwa hiyo hakuna excuse pale tunapokosea , tunatakiwa kuwa waaminifu kwa kweli yote,
Tuombe Mungu atusaidie kuwa waminifu zaidi
avatar
Admin
Admin
Posts : 8
Join date : 2018-02-03
https://biblia-yasema.board-directory.net

Lesson Jumapili tar4/2.2018- uaminifu Empty Mwongozo, jumamosi mchana tar 10/2

Sat Feb 10, 2018 1:36 pm
Uaminifu kwa Mungu

Null
SABATO MCHANA

Soma Kwa Ajili ya Somo la Juma Hili:Luka 16:10; Mambo ya Walawi 27:30; Mwanzo 22:1–12; Waebrania 12:2; Luka 11:42; Waebrania 7:2–10, 13; Nehemia 13.

Fungu la Kukariri: “Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia”(Luka 8:15).


Moyo mkweli ukoje, na unadhihirishwaje? Tamaduni za kisasa mara nyingi huutazama uaminifu kama mfumo wa maadili usio dhahiri na wenye kufuata imani kwamba maarifa na maadili ni mambo ya mpito yanayotawaliwa na uwezo wa ubongo na wakati; watu wengi mara chache wanakosa uaminifu lakini wanachukulia kuwa hilo linakubalika maadam uhalifu siyo makubwa sana. Pia mazingira mahususi, inadaiwa, yangeliweza kuhalalisha udanganyifu au kukosa uaminifu kwa kiasi fulani.

Ukweli na uaminifu siku zote vipo pamoja. Lakini bado, hatukuzaliwa na mwelekeo wa kuwa waaminifu; ni uwezo wa kimaadili ambao mtu anajifunza na uko katika kiini cha tabia ya kimaadili ya wakili. Tunapokuwa waaminifu vitu vizuri huja pamoja nao. Kwa mfano, kamwe hakuna hofu ya kukamatwa katika uongo au kulazimika kuuficha. Kwa sababu hii na zingine zaidi, uaminifu ni sifa bainifu yenye thamani kubwa mno ya haiba, hasa katika hali ngumu wakati ambapo jaribu linaweza kuelekeza katika kukosa uaminifu.

Katika somo la juma hili tutajifunza dhana ya kiroho ya uaminifu kupitia kwenye zoezi la kutoa zaka na kuona kwa nini kutoa zaka ni muhimu sana kwa wakili na uwakili.

*Jifunze somo la juma hili ukijiandaa na Sabato ya Februari 17.



Sponsored content

Lesson Jumapili tar4/2.2018- uaminifu Empty Re: Lesson Jumapili tar4/2.2018- uaminifu

Back to top
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum