BIBLIA YASEMA
Would you like to react to this message? Create an account in a few clicks or log in to continue.

Go down
avatar
Admin
Admin
Posts : 8
Join date : 2018-02-03
https://biblia-yasema.board-directory.net

Lesson sabato mchana tr 10/2 Empty Lesson sabato mchana tr 10/2

Sat Feb 10, 2018 1:49 pm
Uaminifu kwa Mungu

Null
SABATO MCHANA

Soma Kwa Ajili ya Somo la Juma Hili:Luka 16:10; Mambo ya Walawi 27:30; Mwanzo 22:1–12; Waebrania 12:2; Luka 11:42; Waebrania 7:2–10, 13; Nehemia 13.

Fungu la Kukariri: “Na zile penye udongo mzuri, ndio wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno, na kulishika; kisha huzaa matunda kwa kuvumilia”(Luka 8:15).


Moyo mkweli ukoje, na unadhihirishwaje? Tamaduni za kisasa mara nyingi huutazama uaminifu kama mfumo wa maadili usio dhahiri na wenye kufuata imani kwamba maarifa na maadili ni mambo ya mpito yanayotawaliwa na uwezo wa ubongo na wakati; watu wengi mara chache wanakosa uaminifu lakini wanachukulia kuwa hilo linakubalika maadam uhalifu siyo makubwa sana. Pia mazingira mahususi, inadaiwa, yangeliweza kuhalalisha udanganyifu au kukosa uaminifu kwa kiasi fulani.

Ukweli na uaminifu siku zote vipo pamoja. Lakini bado, hatukuzaliwa na mwelekeo wa kuwa waaminifu; ni uwezo wa kimaadili ambao mtu anajifunza na uko katika kiini cha tabia ya kimaadili ya wakili. Tunapokuwa waaminifu vitu vizuri huja pamoja nao. Kwa mfano, kamwe hakuna hofu ya kukamatwa katika uongo au kulazimika kuuficha. Kwa sababu hii na zingine zaidi, uaminifu ni sifa bainifu yenye thamani kubwa mno ya haiba, hasa katika hali ngumu wakati ambapo jaribu linaweza kuelekeza katika kukosa uaminifu.

Katika somo la juma hili tutajifunza dhana ya kiroho ya uaminifu kupitia kwenye zoezi la kutoa zaka na kuona kwa nini kutoa zaka ni muhimu sana kwa wakili na uwakili.

*Jifunze somo la juma hili ukijiandaa na Sabato ya Februari 17.



Back to top
Permissions in this forum:
You cannot reply to topics in this forum